Na Oliva Casian
Wagombea wakuu wa upinzani kwa nafasi ya Urais katika jamuhuri ya kidemokrasia ya congo, upinzani umetishia maandamano ya kupinga mfumo wa kura kwa mashine za elektroniki kwenye uchaguzi mkuu Desemba 23, upinzani ulisema kuwa wanapinga pia daftari la wapiga kura wasio na alama za vidole kwenye kadi zao.
Hata hivyo, Martin Fayulu mmoja wa wagombea urais ambaye alisoma taarifa hiyo ya pamoja ya upinzani mbele ya waandishi wa habari mjini Kinshasa, alisema upinzani hauna nia ya kuususia uchaguzi huo.
"Tunawatolea wito raia wa Congo kujipanga kwa ajili ya kulazimisha kuweko na kura ya makaratasi kulingana na sheria ya uchaguzi na kalenda iliyotangazwa na tume huru ya uchaguzi".
Licha ya hayo wapinzani walisema wanaunga mkono juhudi zozote za mazungumzo ili kupata suluhisho kuhusu mfumo wa uchaguzi wa matumizi ya mashine ya kielektroniki,taarifa hiyo ya pamoja ya upinzani iliidhinishwa na Vital Karrerhe,Feliy Tshisekedi,Jean-Pierre Bemba,Moise Katimbi,Freddy Matungulu na Martin Martin Fayulu.
Hatua hiyo ya upinzani ilikuja siku moja baada ya kuvunjika kwa mkutano wa pili na tume huru ya uchaguzi (CENI) kujadili changamoto za kiufundi katika maandalizi ya uchaguzi.
Mwenyekiti wa tume hiyo Carneille Nangaa alisema kwamba upinzani ulikwenda na ajenda na masharti yake.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Saturday, October 13, 2018
WAPINZANI WATISHIA KUANDAMANA KUPINGA MFUMO WA UPIGAJI KURA WA KIELEKTRONIKI DRC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Na Sakina Nchila, SABABU SIMBU KUSHINDWA KUMALIZA MBIO MAREKANI. Maumivu hayo yalimfanya simbu kukimbia umbali wa kilometa 30 tu kati ya ...
Post Top Ad
Responsive Ads Here
No comments:
Post a Comment