HOFU YATANDA MAMIA YA WATU HAWAJULIKANI WALIPO BAADA YA MAPOROMOKO YA ARDHI NCHINI UGANDA - STARHABARI

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, October 13, 2018

HOFU YATANDA MAMIA YA WATU HAWAJULIKANI WALIPO BAADA YA MAPOROMOKO YA ARDHI NCHINI UGANDA

Na Oliva Casian
   Zaidi ya watu 50 wamepoteza maisha kutokana na maporomoko ya ardhi na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha mashariki mwa Uganda,mamia ya watu bado hawajulikani walipo huku maafisa katika wilaya ya Bududa wakihofia kuwa idadi ya waliopoteza maisha huenda ikaongezeka.

Walioshuhudia mkasa huo wanasema kuwa mwamba ulidondoka mtoni na kupasua kingo za mto hali iliyosababisha maji yaliyochanganyika na matope kuanza kusamba watu vijijini.

Serikali imesema vikosi vya uokoaji vimepelekwa katika eneo hilo karibuni na mpaka wa Uganda na Kenya lakini miundombinu ya barabara na daraja iliyoharibiwa imelemaza shughuli za uokoaji.

Tukio kama hilo limewahi kutokea eneo hilo la Bududa na kusababisha vivo vya watu 300 mwaka 2010, ambapo Mwanahabari wa kujitegemea Swahib Ibrahim ameiambia BBC kuwa baadhi ya wakazi mpaka sasa hawajui wapendwa wao wako wapi.

Pia Ibrahim amesema kuwa shirika la msalaba mwekundu limekuwa likiwasaidia waathiriwa wa mkasa huo tangu jana.

Kwa upande wake msemaji wa shirika la msalaba mwekundu Irene Nakasiita amesema"Maji yalipoanza kuteremka chini yalibeba mawe makubwa ambayo yaliharibu nyumba za watu" kufuatia mikasa iliyopita watu waliamriwa kuhama eneo hilo lakini wengi wao walirejea kwa kuvutiwa na ardhi yenya rutuba na upendo wa makazi yao ya asili.

No comments:

Post a Comment

Na Sakina Nchila, SABABU SIMBU KUSHINDWA KUMALIZA MBIO MAREKANI.  Maumivu hayo yalimfanya simbu kukimbia umbali wa kilometa 30 tu kati ya ...

Post Top Ad

Responsive Ads Here