WAKAZI WA TABATA MKENGENI WAKUMBWA NA TATIZO LA MMOMONYOKO WA UDONGO.
Na Rachel Emmanuel
Wakazi wa Tabata Mkengeni wakumbwa na tatizo la mmomonyoko wa udongo ambalo limesababishwa na maji yapitayo mto wa msimbazi pindi mvua zinanyeesha ambapo maji hujaa sana kupita kiasi na kupelekea udongo kudondoka na daraja lililokuwa apo awali. Na pia kulkuwapo na barabara limeharibiwa na mto huo na kutengeneza bonde la Ufa. Hivi sasa maji yamekauka na kuacha udongo bado kuwa na maji maji ambao unaosababisha mmomonyoko na nyumba kukaribia kuanguka.
Inasemekana kuwa mto huo ulikuwa mdogo sana yakipitisha maji na kuzungukwa na msitu lakini pindi mvua zilipokuwa zinanyeesha kubwa zilipanua mto huo na kuufanya mkubwa kila siku mpaka kufika hatua ya kuharibu msitu uliokuwa umeuzunguka.
Na haya yote yalianza tangu mwaka 2016 ambapo mvua zilikuwa zinanyeesha bila kikomo na kufanya hali ya wakazi wa apo kuwa ngumu kwa sababu maji yalikuwa yanaingia ndani na kuharibu vitu vyao. Huu mto ulianza Kisarawe na kupita hadi Mkengeni na kuendelea Vingunguti hadi Jangwani ambapo maji huishia apo.
Wakazi wa apo pia walieleza kuhusu suala hili na kusema," tabu ya apa ilikuwa ni jinsi ya kuvuka ule mto maana maji yalijaa hadi sehemu yakupita haikuwepo na vivukio navyo havipo kama daraja maana na lenyewe lilichukuliwa na maji, sasa kwa sababu mvua hamna tena maji yamekauka limebaki tatizo la udongo kwa kuwa umeshiba sana maji na unaanza kulegea na kuanguka hali inayopelekea nyumba zilizoko juu kuwa hatarini." Alisema Cosmas Kaluwa
Na pia Bi Aisha seif aliongeza kuwa," Jambo la apa huwa linatishia amani wakati wa mvua kwa sababu mto huu ndipo unapojaa maji mengi na watu wengi pia walikufa kwakuchukuliwa na maji kutaka kujaribu kuuvuka sasa hivi mvua zilipoacha kunyeesha na mto huu kukauka tukajua tutaishi kwa amani lakini limetokea tatizo hili la udongo kudondoka kwa sababu mto upo chini sisi nyumba zetu zipo juu sasa maji yalikuwa yanajaa na kulainisha udongo huu wa pembeni na kudondoka na wenyewe mto kuendelea kutanuka sasa nyumba zetu zipo hatarini kudondoka."
Nilifanikiwa kuongea na mwenyekiti wa mtaa na kusema washawasilisha kwa viongozi wa juu na kuambiwa wasubiri wataliweka kwenye bajeti hivyo wanalifanyia kazi.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Wednesday, October 3, 2018
Wakazi wa Tabata Mkengeni wakumbwa na mmomonyoko wa udongo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Na Sakina Nchila, SABABU SIMBU KUSHINDWA KUMALIZA MBIO MAREKANI. Maumivu hayo yalimfanya simbu kukimbia umbali wa kilometa 30 tu kati ya ...
Post Top Ad
Responsive Ads Here
No comments:
Post a Comment