- STARHABARI

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, October 4, 2018

MOROCCO NA SHERIA MPYA JUU YA UNYANYASAJI WA KINGONO NA UDHALILISHAJI.
   Na Oliva Casian

Sheria hiyo ambayo inajumuisha upigaji marufuku wa ndoa za kulazimishwa inafuatia kuongezeka kwa hali ya wasiwasi katika miaka ya hivi karibuni juu ya kiwango cha udhalilishaji wanawake,utafiti mmoja unaonyesha wanawake sita kati ya kumi wananyanyaswa.

Hata hivyo sheria hiyo imepokelewa vizuri lakini pia imekosolewa kwasababu ya kutokutoa maana kamili ya unyanyasaji hususani wa majumbani au marufuku katika vitendo vya ubakaji ndani ya ndoa.

Katika Siku hizi za karibuni polisi nchini humo iliwakamata vijana kumi na wawili kwa tuhuma za kumbaka msichana wa miaka kumi na saba na kumtesa katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.

Pia chama cha waandishi wanawake nchini Tanzania(TAMWA)kilisema kwa wastani wasichana wawili kati ya watano huolewa kabla ya kutimiza miaka kumi na nane,na asilimia thelathini na saba(37) ya wanawake wenye umri wa miaka ishirini(20) hadi ishirini na nne(24)walioolewa kabla ya kufikia miaka kumi na nane(18).

Hata hivyo hali hiyo inasadikiwa kupungua huku takwimu zinaonyesha visa vimepungua kwa asilimia kumi tangu mwaka 2004 ambapo viwango vilikuwa asilimia arobaini na moja.

Betty Masanja wakili na mwanaharakati wa masuala ya kijamii nchini alisema"ndoa za lazima zipo sana miongoni mwa jamii hasa watanzania, kuna baadhi ya jamii zinahisi mtu asipoolewa anakosa heshima fulani"

Betty pia ameongeza kwa kusema sheria ya ndoa ya mwaka 1981 haiwalindi wasichana dhidi ya kuolewa mapema.

Kadhalika ipo haja ya kuhamasisha viongozi wa kijamii kuhusu athari za ndoa za lazima na sheria zilizopo ,sekta ya afya ina jukumu kuu la kuwahamasisha wananchi kuhusu athari za ndoa za umri mdogo.

No comments:

Post a Comment

Na Sakina Nchila, SABABU SIMBU KUSHINDWA KUMALIZA MBIO MAREKANI.  Maumivu hayo yalimfanya simbu kukimbia umbali wa kilometa 30 tu kati ya ...

Post Top Ad

Responsive Ads Here