TAFITI;IMF YASEMA UCHUMI WA DUNIA UMESHUKA. - STARHABARI

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, October 11, 2018

TAFITI;IMF YASEMA UCHUMI WA DUNIA UMESHUKA.

Na Oliva Casian
  Shirika la fedha la kimataifa IMF vita vya kibiashara vinavyosababishwa na hatua ya marekani kutanhaza viwango vya ushuru pamoja na madeni makubwa vimeshusha uchumi wa dunia.

Ikitangaza utafiti wake wa hivi karibuni kuhusiana na hali ya uchumi duniani katika kuelekea mkutano wa kilele utakaofanyika Bali Indonesia,IMF kukua kwa uchumi duniani kwa mwaka huu kutasalia katika kiwango cha asilimia 3.7% na kusalia katika kiwango hicho hapo mwakani.

Utafiti huo unaonyesha kuwa kiwango hicho ni cha chini kulinganisha na asilimia 3.4% iliyotangazwa april, uchumi unaonekana kuporomoka na kuwa kiwango cha asilimia 3.7% alisema mchumi mkuu wa IMF Maury Obstfeld wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kutangazwa kwa ripoti hiyo.

Kwa mujibu wa IMF utafiti huu hauhusishi athari ya viwango vingine vya ushuru dhidi ya China vinavyotarajiwa kutangazwa na Marekani pamoja na hatua zitakazochukuliwa na China kibiashara dhidi ya marekani.

Shirika hilo limesema kushindwa kuidhinisha kisheria mikataba ya kibiashara kati ya Marekani,Mexico,na Canada pamoja na mchakato wa Uingereza kujiondoa umoja wa ulaya kuwa moja ya sababu ambazo zinachangia hali hiyo.

Aidha IMF imesema kushuka kwa viwango vya uzalishaji kunaweza kukaiathiri ujerumani kwa kiwango kikubwa mnamo wakati,wakati kiwango cha kukua kwa uchumi wa ujerumani kwa mwaka 2018na 2019 kilikadiriwa kuwa asilimia 1.9% ambacho ni kiwango cha chini na hiyo ikitajwa kusababishwa na kushuka kwa mauzo ya nje pamoja na uzalishaji viwandani.

No comments:

Post a Comment

Na Sakina Nchila, SABABU SIMBU KUSHINDWA KUMALIZA MBIO MAREKANI.  Maumivu hayo yalimfanya simbu kukimbia umbali wa kilometa 30 tu kati ya ...

Post Top Ad

Responsive Ads Here