NEC YATANGAZA TAREHE YA UCHAGUZI SERENGETI NA SIMANJIRO - STARHABARI

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, October 15, 2018

NEC YATANGAZA TAREHE YA UCHAGUZI SERENGETI NA SIMANJIRO

Na Oliva Casian

Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC)imetangaza tarehe ya uchaguzi katika majimbo ya Simanjiro na Serengeti pamoja na kata 21 za Tanzania bara ambapo unatarajiwa kufanyika decemba 2,2018 mwaka huu.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC), jaji wa mahakama ya Rufaa,Semistodes Kaijage ambapo amesema kuwa fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa kati ya tarehe 28 oktoba hadi 03 Novemba mwaka huu.

"Uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 03 Novemba mwaka huu,Kampeni za uchaguzi zitafanyika kuanzia tarehe 04 Novemba hadi tarehe 01 Desemba mwaka huu na siku ya uchaguzi itakuwa ni tarehe 02 Desemba mwaka huu." amesema jaji Kaijage.

Amesema kuwa Tume ilipokea barua kutoka kwa spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha sheria ya Taifa ya uchaguzi ,alitaarifu Tume uwepo wa nafasi 2 wazi za ubunge katika majimbo mawili(2) jimbo la Serengeti lililopo Halmashauri ya Serengeti mkoani Mara na jimbo la Simanjiro lililopo Halmashauri ya Simanjiro mkoani Manyara.

Aidha Kaijage amesema kuwa barua hiyo imepokelewa kufuatia wabunge wa majimbo hayo ambao ni Marwa Ryoba Chacha na James Ole Millya kujiuzulu na kutoka kwenye vyama vyao vya awali, pia tume imepokea taarifa kutoka waziri mwenye dhamana na serikali za mitaa ambaye kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 13(1) cha sheria ya uchaguzi ya serikali za mitaa alitaarifu tume uwepo wa nafasi wazi za madiwani katika kata 21 za Tanzania bara nafasi hizo zimetokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo na kujiuzulu.

Hata hivyo amezitaja kata zenye uchaguzi ambapo ni pamoja na ilboru,Mkinfavini na Oldonyosambu(Wilaya ya Arusha), Engutoto na Olasiti(Manispaa ya Arusha), Hazina(Manispaa ya Dodoma), Chinugulu(Wilaya ya Chamwino), Kasham,Nyakimbili,Kishongo(Wilaya ya Bukoba), Chonyonyo,Ihanda(Wilaya ya Karagwe), Namilembe(Wilaya ya Ukerewe), Ngarenairobi(Wilaya ya Siha), Kyanyari(Wilaya ya Butiama), Beta(Wilaya ya Mkuranga), na Chikola( Wilaya ya Manyoni).

No comments:

Post a Comment

Na Sakina Nchila, SABABU SIMBU KUSHINDWA KUMALIZA MBIO MAREKANI.  Maumivu hayo yalimfanya simbu kukimbia umbali wa kilometa 30 tu kati ya ...

Post Top Ad

Responsive Ads Here