Na. Michelle John
Mbunge wa Babati mjini ambaye pia ni mwenyekiti wa BAWACHA mkoa wa Manyara na mwenyekiti wa umoja wa wabunge kanda ya kaskazini Pauline Gekul amejivua uanachama wa chadema na kujiuzulu nafasi zote za uongozi alizokuwa nazo na kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM).
Gekul ametaja sababu mbili za kufanya maamuzi hayo, ya kwanza ni chama kuwabebesha wabunge mzigo shughuli za ujenzi wa chama.
Gekul aliendelea kusema kuwa kwenye chaguzi ndogo zote zilizofanyika Manyara alitoa fedha zake mfukoni kugharamia, na chama kilileta laki tano tu, licha ya kwamba kinapokea ruzuku ya zaidi ya milioni 300 kwa mwezi.
Pili amesema ni kupigwa majungu na viongozi wenzie, mheshimiwa Gekul anakuwa mbunge wa nane wa upinzani na tisa wa Bunge la 11 la jamhuri ya muungano Tanzania chini ya souls Ndugai kujiuzulu.
Wimbi hili la hama hama ya wabunge hadi sasa ni Lazaro Nyalandu pekee aliyekuwa mbunge wa Singida kaskazini kupitia CCM alijiuzulu na kujiunga na Chadema.
Hadi sasa wabunge wa upinzani waliojiuzulu na kutimukiia CCM walikopitishwa na kugombea na sasa ni wabunge ni Maulid Mtulia (kinondoni-CUF) na Dk. Godwin Mollel (Siha-Chadema)
Na wanaosubri kuapishwa ni Mwita Waitara (Ukonga-Chadema) na Julius Kalanga (Monduli-Chadema) huku Zuberi (Liwale-CUF) huenda akaibuka mshindi katika uchaguzi uliofanyika.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Monday, October 15, 2018
CHADEMA YAENDELEA KUPATA PIGO, MBUNGE MWINGINE AONDOKA NA KUJIUNGA NA CCM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Na Sakina Nchila, SABABU SIMBU KUSHINDWA KUMALIZA MBIO MAREKANI. Maumivu hayo yalimfanya simbu kukimbia umbali wa kilometa 30 tu kati ya ...
Post Top Ad
Responsive Ads Here
No comments:
Post a Comment