Na. Sakina Nchila
Mahamaka ya Kisutu jijini Dar es Salaam imemsomea mashtaka mawili Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe ikiwemo la kutoa taarifa ya uongo kwa TRA kuhusiana na nyasi bandia, kwa kutaja bei kubwa zaidi.
Inadaiwa kati ya Machi 10 na Septemba 30, 2016, Aveva, Kaburu na Hans Poppe waliwasilisha nyaraka za uongo kuonyesha Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya dola za Kimarekani 40,577 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 90 za Kitanzania.
Baada ya kusomewa mashtaka yao mahakama ilitoa masharti ya dhamana kwa Hans Poppe yaliyomtaka kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya shilingi milioni 15 kila mmoja masharti ambayo ameyatimiza na kupewa dhamana, Kesi hiyo imeahirishwa hadi Ijumaa Oktoba 19 itasikilizwa.
No comments:
Post a Comment