SERIKALI YA UGANDA IMEWATAKA WATU WA WILAYA BUDUDA WAHAME APO KUTOKANA NA MAPOROMOKO - STARHABARI

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, October 16, 2018

SERIKALI YA UGANDA IMEWATAKA WATU WA WILAYA BUDUDA WAHAME APO KUTOKANA NA MAPOROMOKO

Na. Sakina Nchila
      Serikali ya Uganda imewataka watu wa wilaya ya Bududa mashariki mwa Uganda wahame kutoka kijiji cha Bukalasi na vijiji vyengine vilivyoko kwenye wilaya ya Bududa kutokana na maporomoko ya mawe.
Mvua kubwa ilionyesha siku ya Alhamisi iliopita ilisababisha uharibifu wa majumba mengi na kusababisha vifo vya wattu takriban 50 huku miili ikiendelea kupatikana.

Kuna hofu ya kutokea maradhi ya kuambukiza kutokana na maiti zinazo patikana katika Mto Sume na mto Manafwa baada ya mvua hiyo kubwa.


Rais Yoweri M7 amewafariji na kuwapa pole wakaazi wa wilaya hiyo ya Bududa wanaofikia 250,000 na amesema atawapa Sh Million 5 za Uganda kila familia iliopoteza mtu wake na Sh Miilion 2 kwa kila aliejeruhiwa .
Wakaazi wengi wa Wilaya ya Bududa wanaonekana sasa kukubaliana na mpango wa Serikali licha ya baadhi kuitaka serikali iwahakikishie zoezi hilo litafanyika.

Baadhi ya watu waliohamishwa na kupelekwa eneo la Kiryandongo 2010 wamekua wakilalamika kuhusu ugumu wa maisha huko na hali wengine wamekatazwa kuishi Kiryandongo kwa sababu hawajulikani katika ofisi kuu ya waziri mkuu wa Uganda.
Hata hivyo rais Museveni amewambia watu wa Wilaya ya Bududa njia peke sasa nikuwahamisha watu wote kutoka eneo la Bududa.
Serikali ya Uganda tayari imeweza kuhamisha familia za watu zaidi ya 600 na kuwapa ardhi ya kukaa na kulima na pia Waziri Mkuu Ruhakana Rugunda amesema serikali imetumia Sh Billion 8 kununua ardhi nyengine eneo la Bulambuli.
Serikali sasa inafanya mipango hatua kwa hatua kuanza kuwahamisha watu wote kutoka wilaya ya Bududa rasili mali zitakapo patikana .

Sir Bob Moshikori Mfalme wa Masaba eneo la Bugisu ameitaka serikali na watu wote wa kabila la masaba walioko Uganda na hata walioko nchini Kenya wote wajitokeze kwa hali na mali kuwasaidia ndugu zao wa wilaya ya Bududa Mfalme alikozaliwa.
Mzee Patrick Namukobe alipoteza watoto 6 katika maafa ya mwaka 2010 na bado anauchungu sana serikali kushindwa kuwahamisha na kuwapeleka Bulambuli, lawama nyingi akiwatupia baadhi ya wabunge wa eneo hilo.

Diwani wa wilaya ya Bukalasi Shibale Milton lilopoteza watu wengi kwenye maafa ya Alhamisi, amesema walikubali kuondoka Bududa tangu mwaka 2010 watu walipo fariki eneo la Namutsi lakini amesema wanasiasa ndio wamekua wakikwamisha zoezi la kuwahamisha.

No comments:

Post a Comment

Na Sakina Nchila, SABABU SIMBU KUSHINDWA KUMALIZA MBIO MAREKANI.  Maumivu hayo yalimfanya simbu kukimbia umbali wa kilometa 30 tu kati ya ...

Post Top Ad

Responsive Ads Here