- STARHABARI

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, September 29, 2018

Dar es salaam

Na.Muhamedi Athumani

   Waziri wa mifugo na uvuvi Luhaga Mpina ameunda tume ya kiukaguzi ya kiuchunguzi ili kufanya ukaguzi wa kina wa hesabu za fedha katika soko la kimataifa la feri jijini dar es salaam baada ya uongozi wa soko hilo kudaiwa kutumia vibaya kiasi cha sh. Milioni 100 zinazokusanywa kila mwezi katika soko hilo.

Amesema hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara na wavuvi katika soko hilo ambapo alisema kuwa hajaridhishwa na matumizi ya fedha hizo kwakuwa amefanya ukaguzi wa miundombinu ya soko na kubaini ni mibovu na michafu huku mifereji ya maji machafu ikitoa harufu mbaya na kuwakera wateja wanaofika sokoni hapo.

Alisema mbali na tume hiyo kufanya ukaguzi wa hesabu za fedha pia tume hiyo itakayoundwa na maafisa wa wizara ya mifugo na uvuvi kwa kushirikiana na ofisi ya raisi tamisemi itafanya kazi hiyo ndani ya siku saba.

Aidha mbali na hayo alisema  "kuanza sasa watumishi  wa wizara yake watakaa kwenye soko hilo na watashiriki katika kuongoza menejimenti ya soko hilo na mialo yote isiyo rasmi ifutwe na kuondolewa ili kupita kwenye mialo rasmi inayokubalika kisheria,"alisema mpina.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya ilala sophia mjema alimshukuru waziri mpina kwa kufika sokoni hapo na kusikiliza kero za wafanyabiashara na wavuvi na kumhakikishia kuwa maagizo yote aliyotoa atayasimamia kikamilifu ili soko hilo liweze kutoa mchango unaostahili katika nchi.

No comments:

Post a Comment

Na Sakina Nchila, SABABU SIMBU KUSHINDWA KUMALIZA MBIO MAREKANI.  Maumivu hayo yalimfanya simbu kukimbia umbali wa kilometa 30 tu kati ya ...

Post Top Ad

Responsive Ads Here