Na. Rachel Emmanuel
Kaburi lenye miili ya watu 75 limegunduliwa nchini Libya. Miili hiyo inashukiwa kuwa ya wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS.
Maafisa nchini Libya wamegundua kaburi hilo karibu na mji wa pwani wa Sirte ambao hapo zamani ulikuwa ngome kuu ya kundi hilo la itikadi kali katika Afrika kaskazini.
Msemaji wa jeshi la nchi hiyo katika eneo la Benghazi, Salem el Ameel amesema mkazi mmoja aliripoti kuhusu kaburi hilo mwezi mmoja uliopita katika shamba wilaya ya Al-Daheir, mashariki mwa Sirte.
Ameongeza kwamba wale waliopatikana katika kaburi hilo wanonekana kuwa wamevaa nguo za wapiganaji wa IS, lakini uchunguzi wa kitaalamu unahitajika kubaini wao ni nani na wanatoka wapi.
Katika tukio jingine, jeshi hilo linalojitambulisha kuwa jeshi la taifa la Libya limesema limekamata meli mbili za uvuvi za italia katika pwani ya Libya.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Saturday, October 13, 2018
ZAIDI YA MIILI YA WATU 75 YAKUTWA KATIKA KABURI MOJA NCHINI LIBYA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Na Sakina Nchila, SABABU SIMBU KUSHINDWA KUMALIZA MBIO MAREKANI. Maumivu hayo yalimfanya simbu kukimbia umbali wa kilometa 30 tu kati ya ...
Post Top Ad
Responsive Ads Here
No comments:
Post a Comment