CHUO CHA UFUNDI STADI (VETA) KIMEMUENZI BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS NYERERE KWA KUKARABATI GARI ALILOKUWA AKILITUMIA ZAMANI - STARHABARI

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, October 13, 2018

CHUO CHA UFUNDI STADI (VETA) KIMEMUENZI BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS NYERERE KWA KUKARABATI GARI ALILOKUWA AKILITUMIA ZAMANI

Na. Rachel Emmanuel

Chuo cha ufundi stadi (VETA) kimemuenzi baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa kulifanya ukarabati gari alilokuwa akilitumia wakati wa harakati za kutafta uhuru wa tanganyika.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi mkuu wa VETA nchini; Dr Poncras Bujulu, wakati wa maonyesho ya wiki ya vijana ambayo kitaifa inafanyika mkoani Tanga.

Dr Bujulu amesema wameamua kulikarabati gari hilo ili kumuenzi hayati Mwalimu Nyerere ambapo kazi hiyo imefanywa na vijana na vijana wanaopata mafunzo ya ufundi stadi kutoka Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Gari hilo aina ya Austene kama unavyoiona apo chini ina namba ya usajili ms 5480, inahisiwa lilitengenezwa mwaka 1947, lilikuwa limehifadhiwa kwenye ofisi ya chama cha mapinduzi (CCM), mkoa wa Kilimanjaro.

"Kwetu ilikuwa kama fursa kwa vijana wetu namna walivyoiva kwenye ufundi tukaliomba na kupatiwa na kwa sasa tumelitengeneza na linatembea," amesema Mkurugenzi huyo

Kwa muhimu Dk. Bujulu, gari hilo lilitumiwa na Mwalimu Nyerere mwaka 1961 wakati wa harakati za kutafuta uhuru.

Gari hilo linatarajiwa kukabidhiwa kwa serikali oktoba 14, siku ya kilele cha maonyesho hayo.




No comments:

Post a Comment

Na Sakina Nchila, SABABU SIMBU KUSHINDWA KUMALIZA MBIO MAREKANI.  Maumivu hayo yalimfanya simbu kukimbia umbali wa kilometa 30 tu kati ya ...

Post Top Ad

Responsive Ads Here