RAIS MAGUFULI AIPATIA TAIFA STARS KIASI CHA SHILINGI MILIONI 50 - STARHABARI

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, October 19, 2018

RAIS MAGUFULI AIPATIA TAIFA STARS KIASI CHA SHILINGI MILIONI 50


Na Oliva Casian
Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli amekabidhi fedha taslimu shilingi milioni 50 kama alivyoahidi kwaajili ya kusaidia maandalizi ya Taifa Stars kuelekea mchezo wake wa Kufuzu Afcon dhidi ya Lesotho utakaopigwa Novemba 18, 2018. 

”Nawachangia milioni 50 ili iwasaidie katika maandalizi dhidi ya mechi yenu na Lesotho, muhakikishe zinatumika kwa watu wanaotakiwa kwenda”  Rais Magufuli. 

Amesisitiza kuwa atafuatilia matumizi ya kila senti katika fedha hizo na watakaozitafuna watazitapika. 

Ameitaka Taifa Stars kuleta ushindi bila visingizio vyovyote akiwasihi wachezaji kuwa kitu kimoja, kuuchukulia mchezo huo kama vita na kupambana kwaajili ya taifa lao.

No comments:

Post a Comment

Na Sakina Nchila, SABABU SIMBU KUSHINDWA KUMALIZA MBIO MAREKANI.  Maumivu hayo yalimfanya simbu kukimbia umbali wa kilometa 30 tu kati ya ...

Post Top Ad

Responsive Ads Here