RADI YAUWA WANAFUNZI SITA MKOANI GEITA - STARHABARI

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, October 18, 2018

RADI YAUWA WANAFUNZI SITA MKOANI GEITA



Na Oliva Casian
Wanafunzi sita kati ya 25 waliopigwa na radi katika shule ya msingi Emaco Vision English Medium Mkoani Geita, wamekufa katika hospitali ya mkoa walikolazwa kwaajili ya matibabu.

Wakati tukio hilo likitokea, wakala wa jiolojia Tanzania (GST) wametoa mwito kwa jamii na wajenzi wa majengo nchini kuhakikisha wanaweka vizuia radi kwa majengo yote hata kama hayana umeme ili kuepusha madhara ya radi kwa binadamu na mali.

Akizungumzia tukio hilo kaimu mkuu wa mkoa wa Geita,Joseph Maganga alisema taarifa za awali alizopata saa nne hapo Jana ni kwamba radi hiyo iliwajeruhi watoto 25 ambao walikimbizwa hospitali ya mkoa kwaajili ya matibabu.

"Nilipata taarifa kuhusu tukio hilo ingawa niko likizo kidogo ila nilifuatilia na kupewa taarifa hiyo , tumepoteza watoto wetu wadogo sita hadi sasa na taarifa zaidi tutaendelea kuzitoa kadri hali itakavyokuwa , ila ni kweli radi ilipiga na kuleta maafa hayo". Alisema Maganga.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo alisema majeruhi wanaendelea na matibabu hospitalini hapo. Akifafanua zaidi Maganga alisema tukio hilo liliwakumba wanafunzi wa darasa la pili na tatu na pia walimu wawili walijeruhiwa.

Fundi sanifu jiolojia wa GST Christina Andrea alisema Tanzania imepakana na Jamuhuri ya Congo(DRC) ambayo ni kitovu cha radi kwa nchi za Afrika Mashariki na kati, Andrea alisema DRC inaongoza kwa kuwa na radi nyingi na athari za radi hiyo zimeikumba mikoa ya magharibi mwa Tanzania ya Geita,Kigoma, Kagera na Rukwa.

No comments:

Post a Comment

Na Sakina Nchila, SABABU SIMBU KUSHINDWA KUMALIZA MBIO MAREKANI.  Maumivu hayo yalimfanya simbu kukimbia umbali wa kilometa 30 tu kati ya ...

Post Top Ad

Responsive Ads Here