MAISHA YA VICTORIA KIMANI BAADA YA KUONDOKA CHOCOLATE CITY - STARHABARI

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, October 31, 2018

MAISHA YA VICTORIA KIMANI BAADA YA KUONDOKA CHOCOLATE CITY



Na Oliva Casian
Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Victoria Kimani amesema haoni tofauti ya kufanya ndani ya lebo na kufanya pekee yake. 

Vitoria ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Highest Calibre amesema hayo akizungumza na XXL ya Clouds FM. 

"Mimi ni mchapakazi hivyo sioni tofauti kati ya kuwa kwenye management au kufanya kazi bila management, sipo kwenye management ya Chocolate City, kwa takribani miaka miwili na nusu"  amesema Victoria Kimani 

Victoria Kimani ameshafanya kazi na wasanii kadhaa wa Tanzania kama Diamond Platnumz, Ommy Dimpoz na Stereo.

No comments:

Post a Comment

Na Sakina Nchila, SABABU SIMBU KUSHINDWA KUMALIZA MBIO MAREKANI.  Maumivu hayo yalimfanya simbu kukimbia umbali wa kilometa 30 tu kati ya ...

Post Top Ad

Responsive Ads Here