DELE ALLI KUONGEZA MKATABA TOTTENHAM HADI MWAKA 2024 - STARHABARI

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, October 30, 2018

DELE ALLI KUONGEZA MKATABA TOTTENHAM HADI MWAKA 2024

Na. Rachel Emmanuel Tsj

Kiungo wa kimataifa wa England, Dele Alli ameongeza mkataba wa miaka sita ndani ya klabu yake ya Tottenham Hotspur utakaomfanya kuendelea kusalia hapo mpaka mwaka 2024.

Alli ambaye mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kufikia tamati mwaka 2022 ameamua kufikia makubaliano ambapo kwa sasa utamalizika 2024.
Kiungo huyo sasa akitarajiwa kupokea kiasi cha pauni 50,000 kwa wiki huku akipata nafasi ya kuingia kwenye mchezo waliyofungwa 1 – 0 dhidi ya Man City akitokea kwenye majeraha.
Alli mwenye umri wa miaka 22 amejiunga na Spurs kwa dau la pauni milioni 5 akitokea MK Dons mwaka 2015 huku akifanikiwa kufunga jumla ya mabao 48 kwenye michezo yake 153 aliyocheza.

Licha ya kijana huyo kutokuwa na mafanikio ya makubwa ya kutwaa mataji lakinia amewahi kutajwa kuwa mchezaji bora kijana wa mwaka PFA.

Lakini pia ni miongoni mwa wachezaji  waliyopo kwenye kikosi cha meneja Gareth Southgate kilichofanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia baada ya kushinda jumla ya m,abao 2 – 0 dhidi ya Sweden.

No comments:

Post a Comment

Na Sakina Nchila, SABABU SIMBU KUSHINDWA KUMALIZA MBIO MAREKANI.  Maumivu hayo yalimfanya simbu kukimbia umbali wa kilometa 30 tu kati ya ...

Post Top Ad

Responsive Ads Here